Adiuta Biz Assistant – Msaidizi wako katika Biashara

Bila shaka utakuwa umewahi kujaribu kufanya biashara au kwa sasa wewe ni mfanya biashara. Iwe kuuza nyanya gengeni, kuuza soda kwenye kioski, kumiliki kampuni au namna biashara nyingine yeyote. Kati ya mambo ulijifunza ni kuwa kila biashara inahitaji usimamizi ili ikue. Kutoka Shilingi mia moja mpaka kufikia bilioni moja kuna milima ya kupanda na mabonde mbalimbali ya kuyavuka. Moja ya mlima wa msingi sana wa kupanda ni usimamizi wa Biashara yako.

Ninaposema usimamizi simaanishi uwepo wako kwenye biashara. Unaweza kuwepo kwenye biashara, na ukawa unauza mwenyewe, na bado uka hauisimamii biashara. Kusimamia biashara ni pamoja na kujua kila kitu kinachoendelea katika biashara yako: Mapato yako, matumizi, madeni na mali ulizo nazo. jambo hili linakuwa gumu zaidi pale unapotamani kujua mapato yako mengi yanatokea upande upi, ili kuweka nguvu katika upande huo, na tena unapotaka kujua unatumia sana wapi, ili kama kuna uwezekano, upunguze matumizi na kukuza faida. Lakini si hivyo tu, ili kusimamia biashara yako kikamilifu, unapaswa kujua ni wapi unanunua bidhaa au huduma na inakugharimu kiasi gani. Hii itakusaidia kujua kama kuna umuhimu wa kubadilisha unaponunua ili kuongeza faida.

Mali bila daftari hutumika na kwisha bila habari

Wengi wa wafanyabiashara hutumia madaftari kutunza kumbukumbu zao, na wengi wameridhika na hilo. Tatizo ni kwamba, daftari halikupi picha ya biashara yako kwa kipindi chochote utakachokitaka. Lakini pia daftari linaweza kupotea, kuungua au kudhurika hata tu kwa kumwagikiwa na maji. Kwa hiyo njia hii si tu haikusaidii kwenye kusimamia biashara bali sio salama hata kwa taarifa zako.

Wafanyabiashara wengine hutumia Spreadsheets kama Excel. Hizi zinaweza kukupa ripoti mbalimbali za usimamizi wa biashara na ni njia bora kuliko daftari. Lakini njia hii ina mapungufu mengi. Mathalani huwezi kutengeneza na kutuma Ankara (Invoice), hati ya madai (Bill) moja kwa moja toka katika Excel. Pili ili kuweza kuitumia kwa ufanisi kufanya vitu ambavyo ni tata, unapaswa kuwa na ufahamu wa kutosha wa Excel, kitu ambacho wengi wa wajasiliamali hawana. Lakini tatu, usalama wa taarifa ni mdogo, na nne hairuhusu mtu zaidi ya mmoja kuitumia wakiwa maeneo tofauti. Kwa sababu hizi, njia hii pia sio bora kwa wafanyabiashara wanaotaka kuendesha biashara zao kwa akili na ufanisi (Smart and Efficient Business).

ADIUTA BUSINESS ASSISTANT – SULUHISHO LA TATIZO

Baada ya kukumbana na matatizo tajwa hapo juu, sisi pia kama wajasiliamali tuliona kuna haja ya kutengeneza programu ambayo itakuwa suluhu ya matatizo haya. Adiuta Business Assistant (Adiuta BA) ni programu yenye mfumo wa uhasibu (Accounting Package) pamoja na ule wa Orodha na Mauzo (Inventory and Sales) ambazo kwa pamoja zinawawezesha wafanyabiashara, wakubwa kwa wadogo, wa kada zote za biashara, kuweza kufanya biashara zao kwa ufanisi kwa kupata picha halisi ya biashara kwa muda mfupi sana.

Adiuta inakusaidia kutengeneza na kutuma Ankara kwa wateja wako, kurekodi Hati za madai (Bili) ambazo biashara yako inadaiwa. Si hivyo tu, Adiuta inakupa uwezo wa kurekodi miamala ya Benki, na kufanya upatanisho wa akaunti zako za Benki (bank reconcilliation). Kwa upande wa Mauzo na Orodha, Adiuta inakuwezesha kutengeneza na kutuma Hati za Manunuzi (Purchase order), kurekodi manunuzi uliyopokea, na kuuza bidhaa zako.

Ili kuhakikisha bidhaa zako haziharibiki, Adiuta ina kuongoza wakati wa kuuza bidhaa zako uanze na ipi, ili zilizo karibu kuharibika ziuzwe kwanza. Lakini pia inakupa hali ya bidhaa (Stock balance) na ripoti maalum ya muda wa kuharibika (Expiring Items Report).

Lakini pia, ili kuhakikisha hauishiwi na bidhaa katika biashara yako, Adiuta inakupa namna ya kuweka viwango vya chini (Re-order levels) ambapo itakupa maonyo mbali mbali kwenye hali ya bidhaa (Stock balance) pale viwango hivi vinapofikiwa.

Adiuta inakupa pia uwezo wa kufuatilia Madeni kwa kukupa ripoti maalum ya umri wa madeni ya wateja wako (Aging receivables), na umri wa madeni unayodaiwa (Aging payables). Kwa namna hii unaweza kujua uanze kufuatilia deni lipi na pia kwa upande mwingine, uanze kulipa deni lipi.

Kwa ajili ya hesabu zako, Adiuta inakupa uwezo wa kusimamia biashara yako kihasibu ikikupa ripoti za kihasibu kama Trial Balance, General Ledger, Statement of Profit and Loss, na Balance Sheet. Pia inakupa uwezo wa kurekodi mali na madeni (Fixed Asset register and Liabilities) na kuthaminisha mali (Assets Depreciation). Ukiwa na Adiuta unaweza kuingiza “Manual Journal Entries” na kufanya mambo mengine ambayo yatairahisishia kazi idara yako ya fedha.

Biashara yako inakusababisha utembee sana? Usijali! Adiuta inakupa uwezo wa kuingia kwenye Simu yako na kufanya miamala muhimu ukiwa popote pale duniani kupitia Mobile app ambayo inapatikana Playstore. Unataka kuongeza mhasibu na mtu mwingine anayehusika na biashara yako? Tumekusikia! Adiuta inakupa uwezo wa kualika mpaka watu watano, katika bishara yako, kitu ambacho kitakuwezesha kuongeza mtu atakayekuwa anaingiza taarifa, mhasibu na pengine msimamizi wa fedha. Adiuta inakuwezesha kuwapa mamlaka tofauti kadri ya mgawanyo wa majukumu yao.

Kiufupi ukiwa na Adiuta Business Assistant una uwezo wa kuona biashara yako na inavyokwenda, hivyo kukuwezesha kuchukua hatua muafaka za kukuza biashara yako. Pale unapopata tatizo, tuna njia mbalimbali za kukuwezesha kuwasiliana nasi kwa msaada wa haraka, na kwa lugha ya kiswahili au kiingereza. Tunajua kuwa unahitaji kuisimamia biashara yako, na tumekuletea jibu la maswali yako!

Unaweza kutengeneza akaunti yako, na kuijaribu Adiuta BA bure kwa kipindi cha siku 30, BONYEZA HAPA kupata akaunti yako na kuanza kuijaribu.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na mhudumu wetu moja kwa moja kupitia kitufe kilichopo chini mkono wako wa kulia. Andika Ujumbe wako hapo na mhudumu wetu atawasiliana nawe. Au BONYEZA HAPA kututumia Email moja kwa moja. Na kwa WhatsApp tuma ujumbe kwenda namba 0767893474. Unaweza pia kutupigia kwa nambari za simu 0673651520 au 0767893474

Kupata taarifa zetu zaidi, tafadhali usiache kutufuatilia Instagram kwa handle ya adiuta_biz.

Kwa usimamizi ulio bora na maamuzi yenye akili, tumia Adiuta Business Assistant!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *